Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Kanuni Za Kufasiri Biblia - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

KANUNI ZA KUFASIRI BIBLIA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
15,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 14, 2024
Product Views:
164
In category:
Sample

Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vitabu vyote duniani. Kwa nini? Ni kwa sababu \\\\\\\\r\\\\\\\\njina lenyewe lina maana ya vitabu au maktaba ya Mungu, yenye jumla ya vitabu \\\\\\\\r\\\\\\\\nsitini na sita. Tena, Biblia ina waandishi wapatao arobaini, waliotumiwa na \\\\\\\\r\\\\\\\\nMungu kuiandika Biblia kwa vipindi tofauti, kati ya muda wa miaka 1500 na \\\\\\\\r\\\\\\\\n1600, wakiongozwa na Mungu mwenyewe, hivyo kuifanya Biblia iwe na\\\\\\\\r\\\\\\\\nmwandishi mmoja tu, yaani Mungu.

DIBAJI

\\\\\\\\r\\\\\\\\nNachukua nafasi hii kumshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kukitoa kitabu \\\\\\\\r\\\\\\\\nhiki mara ya pili ndani ya muda mfupi. Nahesabu kuwa ni neema ya Mungu ya \\\\\\\\r\\\\\\\\najabu kwa ajili ya kitabu hiki kupata mwitikio mkubwa kwa watu wengi sana \\\\\\\\r\\\\\\\\nkupenda kukisoma, hata kuleta hitaji la kukichapisha tena katika muda usiozidi \\\\\\\\r\\\\\\\\nmiaka mitatu. Kusudi la kitabu hiki, ni kuwasaidia wakristo wote wanaopenda \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuisoma Biblia na kuielewa. Kitabu hiki kilichapishwa kwa mara ya kwanza \\\\\\\\r\\\\\\\\nmwaka 2006; na baada ya watu wengi sana kukisoma katika muda mfupi, nilianza \\\\\\\\r\\\\\\\\nkupokea simu nyingi na barua kutoka kwa wasomaji mbalimbali, wakitaka \\\\\\\\r\\\\\\\\nufafanuzi zaidi juu ya mambo kadhaa. Katika toleo la kwanza, nilitoa maandiko \\\\\\\\r\\\\\\\\nmengi zaidi lakini ufafanuzi ukiwa kidogo; nikiamini kuwa msomaji mwenyewe \\\\\\\\r\\\\\\\\natafuatilia maandiko hayo na kuyaelewa. Lakini kutokana na maswali mengi \\\\\\\\r\\\\\\\\nambayo nimeendelea kuyapokea kutoka kwa wasomaji mbalimbali, \\\\\\\\r\\\\\\\\nyalinikumbusha habari ya towashi aliyekutana na Filipo baada ya kutoka kuabudu \\\\\\\\r\\\\\\\\nYerusalemu, alipoulizwa na Filipo kama alielewa kuhusu habari alizokuwa \\\\\\\\r\\\\\\\\nakizisoma juu ya Yesu, alijibu hivi: “Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza?”\\\\\\\\r\\\\\\\\n(Mdo 8:27-35). Hatimaye niligundua kuwa maandiko peke yake bila msaada wa \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuyafafanua, badala ya kuleta majibu, yanazua maswali mengi zaidi. Kwa hiyo,\\\\\\\\r\\\\\\\\nkatika toleo la pili, badala ya kuyataja tu, nimejitahidi kwa kadiri niwezavyo \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuyaelezea, ijapokuwa ni kwa sehemu. Hivyo nakushauri kusoma toleo hili tena,\\\\\\\\r\\\\\\\\nili kupata nyongeza ya maandiko pamoja na maelezo yake. Maandiko na kanuni \\\\\\\\r\\\\\\\\nzilizofafanuliwa katika kitabu hiki, si za kuiga au kusikia kwa wahubiri wengine \\\\\\\\r\\\\\\\\ntu, bali ni kazi ya uchunguzi, utafiti binafsi na ufunuo wa Roho baada ya miaka \\\\\\\\r\\\\\\\\nmingi!

Nilisoma chuo cha theolojia na kuhitimu mwaka 1975. Nilijifunza elimu ya Biblia \\\\\\\\r\\\\\\\\nna unabii na kuiva vilivyo. Kwa muda wa miaka mitano niliendelea na huduma \\\\\\\\r\\\\\\\\nkama mchungaji na mwalimu wa vipindi vya dini mashuleni na vyuoni, pamoja \\\\\\\\r\\\\\\\\nna kuendesha semina za Neno la Mungu kwa watumishi mbalimbali. Katika \\\\\\\\r\\\\\\\\nmaeneo haya yote, nilianza kukutana na maswali mengi ya utafiti wa wanafunzi, \\\\\\\\r\\\\\\\\nambayo yalinipa changamoto kubwa, hata nikajiona kuwa bado nilikuwa \\\\\\\\r\\\\\\\\nsijaielewa Biblia, na hasa kuhusu mafundisho ya wakati wa mwisho ambayo \\\\\\\\r\\\\\\\\nyameleta shida na mgawanyiko miongoni mwa watu wengi.

Katika utafiti wangu binafsi niligundua kwamba, somo kuhusu wakati wa mwisho \\\\\\\\r\\\\\\\\nndilo lililo na maswali mengi sana katika vichwa vya watu wengi, bila kujali ni \\\\\\\\r\\\\\\\\nvijana au wazee; wakristo wachanga au waliokomaa; washirika au wachungaji; \\\\\\\\r\\\\\\\\nwanafunzi wa Biblia au waalimu wa Biblia; wote kwa pamoja wanatatanishwa \\\\\\\\r\\\\\\\\nsana na somo hili. Sababu kubwa ni kukosa kanuni za kuifasiri Biblia, hivyo \\\\\\\\r\\\\\\\\nkukosa uhakika wa kile kinachofundishwa au kuaminiwa. Kila mtu kufasiri kama \\\\\\\\r\\\\\\\\naonavyo yeye mwenyewe, kumesababisha mgawanyiko mkubwa sana wa imani \\\\\\\\r\\\\\\\\nndani ya makanisa mengi, na wengi kutokuwa na uwezo wa kupambanua, lipi ni \\\\\\\\r\\\\\\\\nla kweli, na lipi ni la uongo; lipi ni unabii na lipi lisilo unabii; ni unabii gain \\\\\\\\r\\\\\\\\nuliotimia na ni upi wa kuutazamia n.k

Katika chuo cha theolojia nilichosoma, kulikuwa na mgawanyiko mkubwa sana \\\\\\\\r\\\\\\\\nwa imani, hasa kati ya watumishi wachanga na wale waliotumika kwa muda \\\\\\\\r\\\\\\\\nmrefu. Sisi tulio vijana tuliwahesabu wazee kuwa ni wapinzani na wasiotaka\\\\\\\\r\\\\\\\\nmabadiliko, kwa kuwa mara nyingi tukiwa katika mijadala mbalimbali iliyo nje \\\\\\\\r\\\\\\\\nya madarasa, wazee hao walituonya sana hatari ya kupokea kila fundisho\\\\\\\\r\\\\\\\\nlinalofundishwa chuoni kuwa ni sahihi. Waliyapokea baadhi ya masomo kwa ajili \\\\\\\\r\\\\\\\\nya kujibu maswali katika mitihani tu, lakini si katika mioyo yao, kwa kuwa \\\\\\\\r\\\\\\\\nwaliamini kuwa yalipingana na kanuni za Biblia; hasa yale yaliyohusu unabii na \\\\\\\\r\\\\\\\\nwakati wa mwisho. Lakini tuliwahesabu kuwa ni wapinzani wasiotaka \\\\\\\\r\\\\\\\\nmabadiliko. Pia kulikuwa na tatizo lingine kwamba, hakukuwa na uhuru wa kutoa \\\\\\\\r\\\\\\\\nmaoni kama mwanachuo kuhusu mambo ambayo yalionyesha utata, vinginevyo \\\\\\\\r\\\\\\\\nkungeleta hatari ya kufukuzwa chuoni. Ukweli wa jambo hili nilianza kuuona \\\\\\\\r\\\\\\\\nbaada ya miaka mitano baadaye nikiwa katika huduma; ndipo nilianza \\\\\\\\r\\\\\\\\nkukumbuka maonyo yao, hata kuwakumbuka kwa majina yao, na kuwa sababisho \\\\\\\\r\\\\\\\\nkubwa sana kwangu kufanya uamuzi makini wa kutulia na kujifunza upya.

Jambo la pekee ambalo siachi kumshukuru Mungu daima, ni ile neema \\\\\\\\r\\\\\\\\nniliyopewa kwamba kila nilipofundisha somo ambalo halikubaliani na maandiko, \\\\\\\\r\\\\\\\\nbila kuambiwa au kuonywa na mtu, Roho wa Mungu alinishughulikia vilivyo \\\\\\\\r\\\\\\\\nkiasi cha kukosa amani hata usingizi. Zaidi ya mara moja nakumbuka nilipata \\\\\\\\r\\\\\\\\nkusafiri umbali mkubwa kwa ajili ya kwenda katika makanisa fulani ambayo \\\\\\\\r\\\\\\\\nnilikuwa nimefanya semina, ili kwenda kufanya masahihisho ya mafundisho \\\\\\\\r\\\\\\\\nyangu; hatua hii ilihitaji ujasiri mkubwa! Ndipo nilipoazimia kuacha kabisa\\\\\\\\r\\\\\\\\nkufundisha masomo haya, na kuanza kujifunza upya neno la Mungu pamoja na\\\\\\\\r\\\\\\\\nmaombi. Kazi hii ilinichukua zaidi ya miaka kumi; kuwatafuta waalimu \\\\\\\\r\\\\\\\\nmbalimbali, ili kupata msaada wa kanuni, ambazo zinasaidia kuielewa Biblia, na \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuyapitia upya masomo yangu ya chuo cha Biblia; hii ni pamoja na vitabu vya \\\\\\\\r\\\\\\\\nwaandishi mbambali. Changamoto kubwa niliyoipata kwa wauliza maswali ya \\\\\\\\r\\\\\\\\nBiblia ni hii: Inawezekanaje kitabu muhimu kama Biblia, kifasiriwe na watu \\\\\\\\r\\\\\\\\nbila kutumia kanuni yoyote? Baada ya kazi hii kunichukua muda mrefu, \\\\\\\\r\\\\\\\\nnikiomba na kusoma Biblia, hatimaye Mungu aliniwezesha kwa neema yake\\\\\\\\r\\\\\\\\nkufunguliwa macho ya kiroho na kuanza kuona siri ya maandiko. (Luka 24:44-45;\\\\\\\\r\\\\\\\\nEf.1:17-19). Ndipo nilianza tena kufundisha na kujibu maswali kwa uthibitisho \\\\\\\\r\\\\\\\\nwa maandiko, nikitumia kanuni, ambazo kwa kawaida hazifundishwi katika vyuo \\\\\\\\r\\\\\\\\nvya Biblia; wawe ni wanafunzi wanaochukua Stashahada hata Shahada pia.

\\\\\\\\r\\\\\\\\nNimekutana na watumishi wengi ambao wanakiri kuwa wamekuwa wakifundisha \\\\\\\\r\\\\\\\\nmasomo haya, lakini bila uhakika wowote ila hufundisha kama walivyopokea \\\\\\\\r\\\\\\\\nkwa sababu ya kukosa miongozo muhimu. Wengi wanakiri kufundisha kama \\\\\\\\r\\\\\\\\nwalivyopokea lakini hawawezi kuwa na ufunuo wao binafsi wakiamini kwamba, \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuwa na ufunuo mwingine tofauti na vile walivyopokea ni uasi mkubwa dhidi ya \\\\\\\\r\\\\\\\\nimani za madhehebu yao. Hivyo huwaambia wanafunzi wao kuchagua lile \\\\\\\\r\\\\\\\\nwalionalo kuwa ni jema; huo ni uamuzi mzuri, lakini lililo baya zaidi ni \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuwashurutisha kuamini hata kama hawakubaliani nayo.

Kwa miaka zaidi ya kumi nimeendelea kufundisha chuo cha Biblia. Uchunguzi, \\\\\\\\r\\\\\\\\nutafiti na maswali ya wanafunzi, vimeendelea kuwa changamoto kwangu katika \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuendelea kuisoma Biblia zaidi. Mungu amekuwa mwaminifu sana kujifunua \\\\\\\\r\\\\\\\\nkatika maandiko yake, ili kuthibitisha uhai wa Neno lake. Kumbuka maneno ya \\\\\\\\r\\\\\\\\nmfalme Sulemani alivyosema katika kitabu cha Mithali kuwa, tukimtafuta kama \\\\\\\\r\\\\\\\\nvile tutafutavyo fedha au dhahabu, tutamwona! Kitabu hiki nimekiandika ili \\\\\\\\r\\\\\\\\nkujibu maswali ambayo yanapatikana kwa wakristo wote wa kila mahali katika \\\\\\\\r\\\\\\\\nkanisa la Mungu duniani pote kama vile: Mbingu mpya na nchi mpya ni nini? Je, \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuna mji mtakatifu unaojengwa mbinguni? Je, kutakuwa na kula na kunywa \\\\\\\\r\\\\\\\\ntukifika mbinguni? Je, ni kweli kutakuwa na mashahidi wawili wa kumhubiri \\\\\\\\r\\\\\\\\nYesu baada ya kanisa kuondoka? Wenye uhai na wazee walioko mbinguni ni \\\\\\\\r\\\\\\\\nakina nani? Je, 144,000 ni akina nani? Je, hao ni watu halisi? Je, ufalme wa \\\\\\\\r\\\\\\\\nMungu upo sasa au utakuja baadaye? Je, miaka elfu ni halisi au mfano? Dhiki kuu \\\\\\\\r\\\\\\\\nni kwa ajili ya nani na italetwa na nani? na mengine mengi! Nimejibu maswali \\\\\\\\r\\\\\\\\nhaya yote kwa kutumia kanuni za Kibiblia zilizoainishwa ndani ya kitabu hiki,\\\\\\\\r\\\\\\\\nbila kuruhusu hisia za mwanadamu yeyote au mapokeo ya dini yoyote \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuchukua nafasi, bali Neno la Mungu limejitegemea lenyewe, andiko likifasiri \\\\\\\\r\\\\\\\\nandiko lingine!

Nakualika ndugu msomaji wa Biblia, kufuatana nami kwa kutumia kanuni za \\\\\\\\r\\\\\\\\nkufasiri maandiko zinazoelezwa ndani ya kitabu hiki, pamoja na mifano yote \\\\\\\\r\\\\\\\\niliyotolewa, bila jazba za kiitikadi na chuki za kidini, hata ufikie mwisho wa \\\\\\\\r\\\\\\\\nkitabu. Ukimaliza kukisoma kitabu chote kwa kufuata utaratibu huu, ndipo \\\\\\\\r\\\\\\\\nutaweza kuwa na haki ya kuamua kwa ujasiri kati ya uongo na ukweli. Daima \\\\\\\\r\\\\\\\\nunapopinga jambo, ni vema uwe na sababu za kimaandiko kwa ajili ya ushahidi, \\\\\\\\r\\\\\\\\nbadala ya kupinga tu kwa sababu za kibinafsi au kidini. Kitabu hiki hakifundishi \\\\\\\\r\\\\\\\\nimani ya dini yangu; wala sina mpango wa kuanzisha dini ambayo itafuata \\\\\\\\r\\\\\\\\nmafundisho haya kama wengine wawezavyo kufikiria kwa haraka. Yamkini hata \\\\\\\\r\\\\\\\\nviongozi wa dini yangu hawatakubaliana na mafundisho yaliyomo ndani ya kitabu \\\\\\\\r\\\\\\\\nhiki; lakini ninaamini kuwa hii ni huduma ya kuujenga mwili wa Kristo ulioko \\\\\\\\r\\\\\\\\nduniani. Mungu alivyosema nami kuandika kitabu hiki, sitaweza kusimlia kwa \\\\\\\\r\\\\\\\\nsasa, lakini ninaamini kuwa ukweli uliomo ndani ya kitabu hiki, utajieleza \\\\\\\\r\\\\\\\\nwenyewe. Mungu akubariki sana! 


More Products On Discount
2,000 Tsh. 1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold