Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ufunuo Wa Yohana - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

UFUNUO WA YOHANA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
15,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 11, 2024
Product Views:
128
In category:
Sample

Kitabu cha Ufunuo wa Yohana ni mojawapo ya vitabu muhimu sana ndani ya Biblia, hasa kutokana na sababu ya kuhesabika kuwa ni kitabu kigumu kueleweka, na hivyo kuogopwa kusomwa na watu wengi. Kitabu hiki kinajulikana kuwa ni cha unabii wa agano jipya sawasawa na vitabu vya manabii wa agano la kale. Kinaitwa ni ufunuo kwa sababu maneno yaliyomo ndani yake si ya hekima ya Mungu kupitia \\\\\\\\r\\\\\\\\nmwanadamu kama ilivyo ndani ya vitabu vingine, bali ni maneno na sauti ya Yesu mwenyewe akinena kupitia mtumishi wa Mungu Yohana, huku akimwonyesha funuo mbalimbali na kumwamuru kuandika kila aliloliona na kulisikia, kwa macho na kwa masikio yake.

Kutokana na ufunuo wa Yohana uliomo ndani ya kitabu hiki, kumetokea mafundisho \\\\\\\\r\\\\\\\\nmengi sana yanayotofautiana na kuzaa imani nyingi zinazopingana ndani ya \\\\\\\\r\\\\\\\\nmadhehebu ya aina moja, wakati mwingine hata ndani ya chuo kimoja cha theolojia. \\\\\\\\r\\\\\\\\nTofauti hizi zote zinatokana na kutofautiana katika njia za kufasiri ufunuo, unabii \\\\\\\\r\\\\\\\\npamoja na Maandiko mengine yote. Wengine wanatumia kanuni maalumu \\\\\\\\r\\\\\\\\nzinazowaongoza kupata maana, na wengine hufasiri kwa kutumia historia, jiografia,\\\\\\\\r\\\\\\\\nna pengine kila mtu kudai amepata ufunuo wake binafsi kutoka kwa Mungu. Mambo \\\\\\\\r\\\\\\\\nhaya yote yameendelea kukifanya kitabu hiki kionekane kuwa kigumu sana, na wengi \\\\\\\\r\\\\\\\\nkukiogopa hata kukisoma, wakiamini kuwa ni kitabu kilichojaa siri za Mungu ambazo \\\\\\\\r\\\\\\\\nni vigumu kwa mwanadamu wa kawaida kuzielewa. Hata imekuwa, mtu yeyote \\\\\\\\r\\\\\\\\nakihubiri kutoka katika kitabu hiki, kunatokea mambo mawili: kwanza, mhubiri \\\\\\\\r\\\\\\\\nmwenyewe kutokujiamini katika kile anachohubiri; pili, wasikilizaji kutothamini kile \\\\\\\\r\\\\\\\\nkinachoelezwa kwa sababu wamejenga dhana potofu ya kuwa kitabu hiki hakuna \\\\\\\\r\\\\\\\\nanayekielewa.

Baada ya kufundisha kitabu hiki miaka mingi katika semina mbalimbali pamoja na \\\\\\\\r\\\\\\\\nchuo cha Biblia, nimepata uzoefu mkubwa zaidi kutokana na changamoto mbalimbali \\\\\\\\r\\\\\\\\nzinazotokana na maswali mengi wanayoyapata kwa wahubiri wa Injili wanaohubiri\\\\\\\\r\\\\\\\\nkutoka ndani ya kitabu hiki, lakini hawako tayari kujibu maswali ya wasikilizaji. \\\\\\\\r\\\\\\\\nWengine wanakuwa wameshika mafundisho hayo bila uthibitisho wowote wa \\\\\\\\r\\\\\\\\nmaandiko, na hawako tayari kubadili mtazamo wao hata kama wataona ukweli. \\\\\\\\r\\\\\\\\nKwangu mimi, kumsikiliza kila mtu na imani yake na kufuatilia maeneo ambayo \\\\\\\\r\\\\\\\\nmisingi yake imejengwa katika Biblia, imekuwa msaada mkubwa kwangu kuniongoza \\\\\\\\r\\\\\\\\nkukiandika kitabu hiki ili kuwasaidia wanafunzi wote wa Biblia wanaotaka kujifunza \\\\\\\\r\\\\\\\\nmaandiko kwa uthibitisho wa andiko kwa andiko, bila kuingiza mawazo na fikira za \\\\\\\\r\\\\\\\\nkibinadamu. Kila msomaji sharti ajue kwamba Biblia inaweza kujitafsiri yenyewe bila \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuhitaji msaada wa mawazo ya mtu.

Nimekusudia kukiandika kitabu hiki baada ya utafiti mkubwa wa kujua ni mambo \\\\\\\\r\\\\\\\\ngani hasa yanayosababisha kuwe na ugumu wa kukielewa kitabu cha ufunuo? \\\\\\\\r\\\\\\\\nKusoma na kulinganisha maandiko juu ya kila jambo lililonenwa na kitabu cha \\\\\\\\r\\\\\\\\nUfunuo, nimeweza kugundua kwamba hakuna jambo hata moja lililofunuliwa kwa \\\\\\\\r\\\\\\\\nYohana ambalo lilikuwa jipya na halikupata kusemwa na nabii mwingine yeyote. \\\\\\\\r\\\\\\\\nNdipo nikagundua kuwa kitabu cha ufunuo sio unabii, bali kinathibitisha utekelezaji \\\\\\\\r\\\\\\\\nwa yote yaliyonenwa na manabii.

Tunaposema manabii tuna maana ya waandishi \\\\\\\\r\\\\\\\\nwote wa agano la kale, pamoja na Yesu mwenyewe ambaye ndiye mkuu wa unabii, na \\\\\\\\r\\\\\\\\nbaadhi ya mitume walioandika nyaraka ambao ujumbe wao ulikuwa wa kinabii, na \\\\\\\\r\\\\\\\\ntukitaka kujua utimizo wake, basi tunahitaji kukielewa kitabu cha ufunuo. Hii ni siri \\\\\\\\r\\\\\\\\nkubwa kwa wasomaji wengi ambao wanakisoma kitabu cha ufunuo sawasawa na mtu \\\\\\\\r\\\\\\\\naliyegeuza maandishi juu chini na chini juu. Ukifuata maelezo yaliyomo katika kitabu \\\\\\\\r\\\\\\\\nhiki bila jazba na itikadi za kidini, nakuhakikishia msaada uliofichika kama dhahabu \\\\\\\\r\\\\\\\\nambao utaupata bila gharama wala kutoa jasho. Yafuatayo ni mambo muhimu sana \\\\\\\\r\\\\\\\\nkuyazingatia kabla hujaanza kusoma kitabu cha ufunuo:

More Products On Discount
10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

2,000 Tsh. 1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold