Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Matumaini Yasiyo Na Tija - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

MATUMAINI YASIYO NA TIJA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
17,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 15, 2024
Product Views:
124
In category:
Sample

MATUMAINI YASIYO NA TIJA: Watu wengi wanaaminishwa vitu visivyo vya kweli, karibu ujifunze ukweli ambao utakuweka huru.

DIBAJI

Bwana Yesu asifiwe, wasomaji wote wa kitabu hiki! Kwa mara nyingine tena, namshukuru sana Mungu kwa neema yake juu yangu, kuniwezesha kuandika kitabu kingine katika mfululizo wa vitabu vingine vilivyotangulia. Katika utumishi wangu wa miaka arobaini nikiwa mchungaji na mwalimu wa Biblia, Mungu nameendelea kuniongoza kwa ustahimilivu mkubwa kuyaona mambo mengi sana yakibadilishwa ndani ya neno la Mungu, kutokana na sababu za kutokujua ama za makusudi kabisa, za wahubiri na wachungaji. Kwa kadiri ambavyo makanisa yanaongezeka, na vyuo vya Biblia vinaongezeka, na watumishi kuongezeka; ndivyo kadiri upotofu wa maandiko na ukengeufu miongoni mwa wakristo wengi unavyozidi kuongezeka zaidi na zaidi! Nilipata kuongea juu ya jambo hili na mtumishi wa Mungu mmoja, naye alinikumbusha kwa kusema hivi: „Ni sawasawa na jinsi ambavyo zamani kulikuwa na huduma za afya chache sana, kama vile vituo vya afya pamoja na zahanati; na magonjwa pia yalikuwa machache sana; kadiri huduma za afya zinavyozidi kuenea vijijini, ndivyo kadiri hiyo hiyo magonjwa yanazidi kuenea mijini na vijijini. Jambo hili linatisha sana! 

Huduma za kiroho zilipokuwa chache sana yaani, makanisa machache, wahubiri wachache, waalimu wachache na huduma nyinginezo; maasi na kufuru dhidi ya Mungu zilikuwa chache sana; lakini kwa kadiri huduma za kiroho zinavyozidi kuongezeka, ndivyo kadiri maasi yanavyozidi kuongezeka, na kufuru nyingi sana! Huduma nyingi zimegeuzwa kuwa ni za kibiashara; na kila mtu kutafuta soko la kile anachokifanya, bila kujali kwamba anawapeleka watu kwa Mungu, kusudi ni kutangaza soko la biashara yake. Kwa sababu hii, watu wa Mungu wataangamia kwa kukosa maarifa; kwa sababu Biblia inasema kuwa, yule anayeongoza vibaya, pamoja na wale wanaoongozwa na mtu huyo, wote wataangamia. Vyuo vya Biblia vimeongezeka sana; elimu ya vyeti, stashahada na shahada wengi wamepata, lakini ukweli wa Neno la Mungu unazidi kupotea! Watu wanatumainishwa mambo ya uongo, mambo ambayo hayako. Viongozi wenyewe wameshindwa kuielewa Biblia na kupotosha makundi ya watu kwa uongo. Hali hii imewafanya wakristo wengi kutokuwajibika ipasavyo, lakini wana matumaini makubwa ya kwenda mbinguni pasipo kazi yoyote. Inawezekana kabisa mtu kuyageuza mafundisho yake yaelekee vile anavyotaka, lakini haiwezekani kabisa mtu kuigeuza nia na makusudi ya Mungu yawe kama anavyotaka. Wanahubiri kana kwamba wamewahi kufika mbinguni halafu wakarudi tena duniani. Wanaeleza mambo ambayo hayako katika maandiko, bali yanatoka katika akili zao .

Baada ya kuyachunguza mambo haya kwa muda mrefu sana; kwa neema ya Mungu, nimewezeshwa kuchambua mambo kadha wa kadha ambayo yana utata mwingi katika kuyafundisha, kutokana na lugha zilizotumika, kama vile, lugha za mifano, lugha za mafumbo, lugha wakilishi, lugha za alama, maneno halisi na yale yasiyo halisi, matumizi ya tarakimu na nyinginezo nyingi. Nimetumia vielelezo vingi vya maandiko yanayothibitisha ukweli wa Biblia isemavyo juu ya mambo yanayoshikiliwa na wakristo kutokana na mapokeo tu, lakini si Neno la Mungu. Hatutendi jambo lolote, wala kufundisha jambo lolote kwa sababu sisi tunalipenda, bali kwa sababu jambo hilo liko katika maandiko, na limethibitishwa kwa sababu za kujitosheleza. Jambo lolote unaloliamini na kulifundisha, sharti uwe umelijua vema, na unaweza kulitetea kwa kulitolea sababu za kutosha zinazotoka katika Neno la Mungu; na kwa lugha iliyofasiriwa kwa usahihi wa kanuni ya lugha. Hatufundishi jambo kwa sababu ya kuwaona wengine wanafanya hivyo, bali kwa sababu Neno la Mungu linasema hivyo. Haitoshi kufundisha jambo bila kutoa uthibitisho wa jambo lenyewe katika maandiko. Kuna mafundisho mengi ambayo ni maarufu sana duniani pote, lakini hayana ukweli wowote wala kuthibitishwa katika maandiko. Waalimu wengi wa Biblia hawawezi kusahihisha mafundisho hayo katika vyuo vyao, ijapokuwa wanaweza kuona makosa, lakini kwa sababu ya kuogopa wakuu wa dini, au kwa sababu ya kuogopa kuitwa wazushi, hawawezi kuitetea kweli wanayoijua. Ni lazima kila msomaji wa Biblia ajue kwamba, Mungu hatatia muhuri juu ya yale tunayoyaamini ili yakubalike kuwa ni ya kweli; bali sisi tutayaamini yale yaliyokwisha kutiwa muhuri na Mungu tangu mwanzo. Yesu alisema kuwa, “Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamizamwili na roho katika jehanum.” (Math.10:28)

Ukiwa mchunguzi mzuri wa Biblia utatambua kuwa, wale wanaoitwa wazushi wa maandiko, si kwamba kila jambo wanalolifundisha ni la uongo; bali ni kwa sababu baadhi ya yale wanayoyafundisha hayamo katika mitaala inayotambuliwa na vyuo vyote duniani. Kuna mafundisho mengi yanayojulikana duniani ambayo hata mimi nilijifunza katika chuo cha theolojia na kuyashika vizuri; lakini kila nilipofundisha, Mungu alinipa neema ya ajabu kwamba usiku huo sikuweza kupata usingizi kabisa kwa kukosa amani. Ndipo nilianza kuyapitia upya kwa kuomba na kusoma kwa uthibitisho wa maandiko. Kazi hii ilinichukua zaidi ya miaka kumi kabla sijaanza kufundisha tena kwa uhuru na uhakika. Moja ya utafiti nilioufanya kwa muda mrefu, ni kuongea na waalimu wa vyuo vya Biblia na kutafuta usahihi wa maandiko. Hatimaye nilitambua kuwa, hata waalimu wengi wa Biblia hufundisha mambo bila uhakika, ila kwa sababu tu nao walifundishwa hivyo. Hii ni hatari! Ni maombi yangu kwa Mungu kwamba, wewe utakayebahatika kukipata kitabu hiki; ukisome kwa utulivu bila jazba, na kuweka kando itikadi yako ya imani ya muda mrefu, kwa kuyafuatilia maandiko yote yaliyoonyeshwa, na sababu zote zilizoainishwa ndani ya kitabu hiki, kwa kuwa zimefanyiwa utafiti wa kutosha, kwa ajili ya kukusaidia wewe; ili baada ya kusoma, upate kuona kwamba wapi kuna ukweli, na wapi kuna upotofu; ili hatimaye uweze kuwa na maamuzi yako yaliyo sahihi juu ya fundisho husika.Nakukaribisha katika jina la Yesu Kristo!

More Products On Discount
5,000 Tsh. 1,000 Tsh.

Sold by: RAMV MRUMA

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.
(0.6)

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold