Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Kuwa Na Uwezo Mkubwa Kiakili - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKILI

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
20,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 23, 2021
Product Views:
1,511
In category:
Sample

AKILI ILIYO SAHIHI: Ina uwezo wa kufumbua matatizo yake. Akili inayohitajika, lazima iwe na uwezo wa kutatua au kufumbua matatizo yake. Kazi ya akili ni kutoa ufumbuzi wa matatizo, au kutoa msaada wa jinsi ya kufanya au kufanikisha jambo fulani. Akili timamu, linapotokea tatizo, hutoa njia ya kulitatua. Lengo tujue kuwa, sio kila akili inafaa, au sio kila akili ni nzuri. Yafaa tujue kuwa kuna aina nyingi za akili, lakini tunachokitafuta kujua akili zilizo bora zaidi ya nyingine. Hakuna maana ya kuwa na akili ambayo ukiwa na tatizo inashindwa kutoa ufumbuzi. Kama una kalikuleta(kikokotoo) lakini unapoipa hesabu haitoi majibu au inachanganyikiwa je kuna maana gani ya kuwa na kalikuleta kama hiyo? Ninacho maanisha hapa ni kukujulisha kuwa, ubora wa akili ni kazi zake inazofanya au iwapo zitamsaidia aliye nazo kufumbulia matatizo yake magumu. akili ni “problems solver: Kwa hiyo basi, inafaa tuupime ubora wa akili katika uwezo wake wa kutoa ufumbuzi kwa mwenye nazo. Neno akili tunaweza kuliita jina lingine nalo ni “Utambuzi” Utambuzi, ni hali ya kugundua au kujua baada ya kutokujua, au kufichua kile kilicho fichika. Akili lazima iweze kutambua vitu ambavyo kwa kawaida ni vigumu kuvijua au kuvipatia utatuzi

"KUWA NA UWEZO MKUBWA KIAKILI"


Ni kitabu maalumu kwako, msomaji wangu, ili kikusaidie katika kukupatia mbinu bora za kukuwezesha kuwa na uwezo mkubwa kiakili(Kuongeza akili na kuzitibu akili, na kuzitumia kwa manufaa). Kitabu kitakusidia kujua nini maana ya akili, na jinsi ya kuziongezea uwezo (Au kuzitunza), na pia jinsi ya kuzitumia vizuri,


Zikuletee matokeo chanya katika maisha yako.
Wazo la kukuandikia kitabu.


Wazo la kukuandikia kitabu hiki limetokana na kitabu
nilichoandika, kiitwacho KUWATUNZA WAZEE NA
VIKONGWE. Baada ya kufanya tafiti za matatizo ya
mabadiliko ya maumbile ya wazee haswa ya kiakili,
ndio kimekuwa chanzo cha kupata wazo hili la kuaandika kitabu maalumu cha kuongeza uwezo wa kiakili.


Nilipokuwa nafanya tafiti zangu nimegundua kuwa watu wengi wanahitaji msaada mkubwa wa kujua jinsi wanavyoweza kuzihudumia akili zao au kuzitunza au kuzisaidia ili ziweze kuleta matokeo makubwa katika maisha yao.


Watu wengi hawajajua umuhimu wa kuzitunza akili zao, aidha hawajui jinsi ya kuzisaidia akili zao ili ziweze kuwa na matokeo ya hali ya juu. Aidha tukija katika masuala ya elimu(wanafunzi), tunaona wanafunzi wengi wanashindwa kufaulu vizuri darasani, lakini chanzo kikubwa ni kushindwa kujua kanuni za kuzifanya akili zao ziwe na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.


Wanafunzi wengi wanashindwa kufaulu kwa sababu ya udhaifu wa akili, au uwezo mdogo wa akili katika kufikiri na kupambanua mambo. Aidha wanafunzi wengi wanakumbwa na matatizo ya kusahau au kutokuzingatia pale wanapofundishwa darasani, hii ni moja ya shida ya udhaifu wa akili


Katika tafiti zangu kadha nimegundua kuwa, kati ya watu 100, wenye uwezo mzuri wa kufikiri wanaweza kuwa asilimia 5% tu. Asilimia nyingine hawana uwezo mzuri wa kufikiri kwa sababu ya udhaifu wa akili zao. Ninaposema udhaifu wa akili sina maana kutokuwa na akili kabisa, hapana. Bali akili zao zimekosa uwezo wa kufanya kazi kama ilivyokusudiwa. Mfano: Iwapo gari injini yake ikiwa na shida inaweza isiwe na ufanisi au hata mwendo wake unaweza kuwa wa pole pole, kwa sababu injini inatatizo. Hali kadhalika iwapo mtu ubongo wake unashida, au umekosa mahitaji yake muhimu ya kuuwezesha ufanyekazi zake sawasawa, nao hautafanya kazi ipasavyo.

More Products On Discount
10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold
5,999 Tsh.

Sold by: Gemwaga Ndege

2,000 Tsh.

Sold by: Lameck Hulilo

5,000 Tsh.

Sold by: Counselor David

6,000 Tsh.

Sold by: BENJAMIN MTAMBO