
Ndoto Yako Inawezekana - Toleo La 2
Ndani ya Kitabu hiki kuna maswali 50 muhimu ambayo kama msomaji atasoma, akaelewa na kuyajibu kwa utulivu na uaminifu – itampelekea kujitambua, kujithamini, kutambua kipawa (talent) yake, wito na kusudi lake duniani na hatima yake ataishi maisha ya furaha, amani, utulivu na mafanikio makuu.\r\n\r\nNdoto yako Inawezekana ni kitabu ameandika kwa watoto wake akiwashirikisha maarifa na uzoefu ambao alipata kutoka kwa baba yake na maisha yake ya kujitafuta na kutafuta kuishi ndoto yake.
Dr Miles Munroe (1954-2014), Mwandishi wa vitabu,\r\nMhubiri na Kiongozi Mshauri, aliwahi kusema kwenye mafundisho yake, “Huwezi\r\nkuinuka juu ya kiwango cha uwezo wako wa kufikiri na kupambanua\r\nmambo. Kubadili maisha yako, lazima ubadili akili, mawazo na fikra zako”.
Dr Munroe anasema, huwezi\r\nkufanya jambo lolote juu (au nje) ya kiwango chako cha kufikiri –\r\nkubadili maisha yako lazima ubadili akili yako na mawazo\r\n(fikra) yako.
Ili ubadili\r\nakili|fikra|mawazo yako, inabidi ubadili taarifa unazopokea, upate\r\nchanzo chenye taarifa sahihi na kamili kwa kile\r\nunatamani kufanya.
Albert Eistein (1879-1955), Mwanasayansi Mjerumani mwenye\r\nasili ya Kiyahudi, alisema, “Hatuwezi\r\nkutatua matatizo yetu kwa kiwango kile kile cha fikra|akili|mawazo tulivyokuwa\r\nnacho wakati tunayatengeneza”
Kumbe basi, 1. Matatizo\r\ntuliyonayo tumeyatengeneza kulingana na kiwango na ubora (uhafifu) wa fikra\r\nzetu, 2. Kuyatatua haya matatizo, lazima tubadili kiwango na ubora wa\r\nfikra zetu tulizonazo, 3. Ukiendelea kujaribu kutatua matatizo yako, kwa\r\nfikra ile ile iliyo yatengeneza, utatengeneza matatizo juu ya matatizo.
Dr Martin Luther King Jnr. (1929 – 1968) alisema, “I have a dream”, kiswahili chake, “Nina Ndoto” au nina wazo, fikra\r\nna picha kichwani mwangu kuhusu maisha ya mbeleni ya mtu mweusi\r\nAmerika.
Dr King Jnr, hakuwaza tu,\r\nalisema, akatangaza wazi juu ya ndoto yake – kwa vile ilihusisha\r\nwatu wengi, akaisema kwa ujasiri usio wa kawaida.
Alitangaza wazi kuwa, wazo\r\nlangu, ndoto yangu, fikra yangu ndio hii. . . akaisema ndoto yake wazi wazi\r\nkila mwenye sikio la kusikia asikie.
Natamani tujiulize maswali\r\nhaya kufuata maisha ya Dr King Jnr.:
_Dr King aliitoa wapi ndoto\r\nhii?
_ni kwa nini ilikuja kwake\r\nsio kwa mwingine?
_kwa nini aliamua kuisema\r\nndoto yake hadharani?
_alitoa wapi ujasiri wa kusema\r\nndoto yake hadharani?
_kwa nini hakuogopa aibu kama\r\nndoto yake haitatimia?
_kwa nini hakuogopa kufa juu maadui\r\nwa ndoto yake?
\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n
Majibu ya haya maswali ndio\r\nsomo kuu la hiki kitabu...endelea kusoma kitabu hiki...!
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza