Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Malaika Ni Watumishi Wetu - GetValueInc
Biashara & Ujasilimia Mali

MALAIKA NI WATUMISHI WETU

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Sep 02, 2021
Product Views:
979
In category:
Sample

Kitabu hiki cha Malaika ni Watumishi wetu, kimelenga kumsaidia kila msomaji na haswa jamii ya Wakristo na watu wote, ili kujua hakika ya uwepo wa Malaika na shughuli za Malaika. Watu wengi wamesikia habari za Malaika na wanajua kuwa Malaika ni kweli wapo, lakini wameshindwa kujua hao Malaika wanakazi gani na wapo kwa ajili gani. Tukija kwa sasa, wacha Mungu ndio kabisa, tumekuwa tukisoma katika maandiko kuhusu Malaika lakini hakuna anayejua kuhusu huduma za Malaika kwa wacha Mungu. Mathayo 4:11.... na tazama, wakaja malaika wakamtumikia. Hapo tumeona maandiko yakisema kuwa, Malaika waliweza kumuhudumia Yesu baada kumaliza mfungo wake wa siku 40. Hii ni wazi kabisa, sio kwa Bwana Yesu tu, bali ni kwa kila mtu aliyemuamini Mungu anayo haki ya kuhudumiwa na Malaika. Unapoendelea kusoma kitabu hiki, pia mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe zaidi katika huduma hii ya ajabu ya Malaika.

MALAIKA NI WATUMISHI WETU

Mamlaka na kazi za Malaika

 

(a)    Mafanikio

Malaika ni mawakala wa mafanikio, kwani na wao huleta kibali na baraka na maongezeko katika maisha ya wanadamu.

Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko; (Mwanzo 24:7)

(b)   Ulinzi

Malaika ni mawakala wa Mungu kutupatia ulinzi. Na hivyo basi hutusaidia kwenye vita vya kiroho pindi tu tunapoomba kwa Mungu na kuwaagiza huingilia kati kutusaidia.

Malaika wa Bwana hufanya kituo, na kuwazungukia wamchao na kuwaokoa (Zaburi 34:7)

Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao watakuchuku, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Zaburi 91:11.12

Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulinde, Zaburi 121:3

Huduma binafsi ya Malaika

Malaika hutuhudumia sisi binafsi. Maelezo mengi katika Biblia huthibitisha kwamba, sisi watu huwa tunashughulikiwa kibinafsi na Malaika. Mimi kama Mwinjilisiti, mara nyingi     nimejiona kwamba sina nguvu za kutosha katika viwanja vya mkutano, ili kusikia ujumbe kwa Bwana, lakini kila mara uchovu wangu hutoweka na nguvu hunirudia tena. Nimekuwa nikijazwa nguvu za Mungu katika nafsi yangu na mwili pia.

Kwa mfano: Eliya 1 Wafalme 19:4.7............Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako.

Mara nyingi Mungu amekuwa halisi kwangu. Akinitumia wageni wake wasioonekana. Yaani Malaika ili waniguse mwili wangu wanifanye niwe mjumbe wake wa mbinguni. Ninene kama mtu afae kwa watu wafao. Hatuwezi kugundua uwepo wa Malaika kila mara. Lakini Malaika huwa jirani zetu. Mara nyingi wanaweza kuwa wenzi wetu pasipo sisi kugundua uwepo wao. Tunajua mambo machache kuhusu huduma yao ya kila mara.

Hata hivyo Biblia hutuhakikishia kwamba, siku moja macho yetu hayatakuwa tena na utando, nasi tutaweza kuona na kujua upeo kamili wa huduma ambayo Malaika wametupa.

Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.(1 Wakorintho 13:11.12)

More Products On Discount
11,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Said Maumba

5,000 Tsh. 4,000 Tsh.
(1)

Sold by: Peter Fabian

25,000 Tsh. 20,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Sellers List
Best Seller
200 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

Best Seller
10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PIUS JUSTUS

Best Seller
25,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold