HOW TO BUILD WEALTH WITH LAND
Jinsi unavyoweza kutengeneza utajiri kwa kupitia kuwekeza katika ardhi
Assume mtu akakupa milioni 5 halafu akakurudisha miaka 20 nyuma na akakupeleka DAR (Dar Es salaam), akakwambia nunua ardhi ambayo miaka 20 ijayo itakutengenezea milioni 500, kwa uelewa ulionao leo utashindwa kweli kuibadili milioni kuwa milioni 500 kupitia kununua maeneo?
Unachakiwa kufanya ni rahisi mno, yale maeneo ambayo sasa hivi yanauzwa milioni 20 mpaka milioni 100, wakati huo ulikuwa unaweza kuyapata kwa laki tano mpaka milioni 1, kwa hiyo ulichokuwa unatakiwa ni kununua maeneo sehemu ambayo unajua baada ya miaka 20 utaweza kuuza kuanzia milioni 50 kupanda juu nadhani hilo unahisi linawezekana ok.
Nikupe test nyingine chukulia umepewa milioni 5 leo ukaambiwa nunua maeneo ambayo miaka 20 ijayo utaweza kuuza milioni 500 utashindwa kweli? Falsafa ni ile ile ambayo utaitumia hapa ni kununua maeneo ambayo unajua miaka 20 ijayo utaweza kuuza kuanzia milioni 100 kupanda juu.
Ukiangalia historia ya bei ya maeneo utagundua ya kuwa kugeuza milioni kwenda milioni 500 kwa kununua maeneo ni kitu ambacho kinawezekana kabisa itakuhitaji uwe mvumilivu tu
Wengi wetu kwa biashara au kwa kazi ambazo tunafanya kufikisha milioni 500 ndani ya miaka 15 au 20 ijayo ni kitu ambacho hakiwezekani
Ila utajisikiaje kama nikikwambia ya kuwa kupitia ardhi unaweza kutengeneza utajiri ambao usingeweza kuutengeneza vinginevyo
Katika kitabu hiki utapata kujua ni kivipi unaweza kugeuza hela kidogo kabisa hata kama ni laki mbili kutengeneza mamilioni ya pesa kupitia ardhi
Utajifunza wapi pa kupata ardhi, na vitu gani ufanye ili uweze kununua ardhi ambayo inaweza kukutengenezea mamilioni hapo baadae