JINSI YA KUUZA UJUZI WAKO
JINSI YA KUUZA UJUZI WAKO
Jamaa mmoja aliulizwa na rafiki zake ni kitu gani alichonacho kinachoweza kumfanya afanikiwe katika maisha? Jamaa akajibu maneno, rafiki zake wakamcheka kwani hawajawahi kusikia mtu akifanikiwa kwa kuwa na maneno tu.
Basi jamaa akaondoka pale akawa akikutana na mtu aliyekata tamaa anamtia moyo, ukihitaji ushauri anakupa ushauri pia akawa anahamasisha watu.
Muda si muda kwa kuwa kazi aliyokuwa anaifanya ilikuwa na msaada kwa watu basi akaanza kulipwa kwa kutoa ushauri na kuhamasisha watu.
Akaanza kuweka maneno yake katika vitabu baada ya kuwa ameona uhitaji ni mkubwa, pia akawa anaweka maneno yake katika sauti na akawa anapata pesa, siku zilivyokuwa zinasogea akaanza kualikwa nje ya nchi kuzungumza, na kupitia maneno yake akafanikiwa kama alivyosema
Je wewe una nini kinachoweza kukufanya ufanikiwe? Unaweza usiwe na ujuzi wa maneno ila ukawa na ujuzi wa aina yoyote ile (na hakuna binadamu asiye na ujuzi), katika kijitabu hiki (kurasa 18 tu) nitakuchukua hatua moja hadi nyingine kukuonyesha namna unavyoweza kuuza ujuzi wako hata kama ujuzi wako unapatikana kila kona.
FALSAFA YA KUUZA MAJI
Ulishawahi kujiuliza kwa nini maji ambayo yanapatikana kila kona na wakati mwingine bure kabisa lakini unaweza kuyanunua kwa TSH 1000 lita moja?
Katika dunia tuliopo unaweza kuuza chochote kile tena kwa bei nzuri ukiwa mjanja, maji yale yale ambao yanapatikana mtaani kuna namna ambavyo unaweza kuyaweka na mtu akawa tayari kununua akiwa na amani zote
Ujuzi wako ambao unaweza kuona ya kuwa hauwezi kuwa na msaada kuna kitu ambacho unaweza kukiongeza na ukauza ujuzi ule ule ambao unapatikana mtaani au kila mmoja anao, unahitaji kujua hatua ambazo zitakuwezesha kuuza ujuzi wako
FALSAFA YA KUUZA GAZETI
Ukifuatilia gazeti linavyoandaliwa unaweza kucheka sana na kujiuliza kwa nini muda wote huu hauku waza kuuza ujuzi wako
Gazeti linakusanya taarifa mbalimbali kutoka maeneo tofauti na hizi taarifa huwa wakati mwingine zinapatikana bure kabisa ila hizi taarifa zinapangiliwa vizuri na zinawekwa kwenye kitu kinaitwa gazeti na mtu anakuwa tayari kununua
Asikudanganye mtu kuwa hauwezi kuuza ujuzi wako, kama taarifa ambazo zinapatikana bure zinauzwa kwa mfumo wa gazeti hata ujuzi wako ambao unadhani hauna maana unaweza kuuza na ndicho nitakachokueleza katika kijitabu hiki cha kurasa 18 tu