SIRI ZA KUISHI NA MWANAUME MKOROFI
Hekima ya kuishi na mwanaume mkorofi
Utoto wa kihisia ni hali ambayo mwanaume amekua kimwili lakini bado hajakomaa katika namna ya kushughulikia hisia zake.
Anaweza kuwa na kazi nzuri, pesa, elimu au umri mkubwa, lakini anapokutana na changamoto za kihisia hutenda kama mtoto.
Hupenda kila kitu kiende anavyotaka, anakasirika haraka, anakwepa kuwajibika, analaumu wengine kwa makosa yake na wakati mwingine hutumia ukimya, vitisho au hasira ili kupata anachokitaka.
Mwanaume wa aina hii mara nyingi si msumbufu kwa sababu ni mbaya kiasili, ila ni kwa sababu hajawahi kujifunza namna ya kudhibiti hisia zake.
Anaweza kuwa alikulia kwenye mazingira ambayo hakufundishwa kuzungumza hisia zake kwa uwazi, alilelewa kwa ukali uliopitiliza au alidekezwa kiasi cha kutokujifunza kuwajibika.
Matokeo yake ni kwamba kila changamoto anayokutana nayo anaiona kama shambulio dhidi yake.
Kujifunza kuishi na mwanaume mwenye utoto wa kihisia ni muhimu sana, kwa sababu ukishindwa kuelewa hali yake, unaweza kutumia nguvu nyingi kupambana naye na kujisahau kwamba hata wewe unapaswa kuishi.
Mara nyingi ugomvi huongezeka pale watu wawili wanapojibu hisia kwa hisia badala ya hekima kwa hisia.
Kuelewa utoto wa kihisia ulio ndani ya mtu kunakupa uwezo wa kutambua kinachoendelea ndani yake ili uchague namna sahihi ya kujibu.
Hekima huanza pale unapoweza kutenganisha tatizo la mtu na thamani yako binafsi.
Kumbuka, ukomavu wa kihisia ni msingi wa mahusiano yenye amani.
Pale ambapo mmoja bado ni mtoto kihisia, mwenzake atalazimika kubeba mzigo mkubwa kwwnye hayo mahusiano.
Hivyo kitabu hiki kitakusaidia kupunguza mzigo huo na kukusaidia na kukuonyesha namna ya kuishi na mwanaume huyo bila kujipoteza na kupoteza furaha yako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza