USIKATE TAMAA, LIPO TUMAINI
Matumaini ni zawadi ya ajabu kutoka kwa Mungu, ni chanzo cha nguvu na ujasiri usoni pa majaribu makali ya maisha. Wakati maisha yanaumiza na ndoto zinafifia, hakuna kinachosaidia kama matumaini. Matumaini ni kitu cha muhimu sana kwetu kama iliyo kwa maji kwa samaki, na umeme kwa balbu. Matumaini ni msingi kwa maisha. Imewahi kusema hivi, kwamba, mtu anaweza kuishi siku arobaini bila ya chakula, siku nne bila maji, dakika nne bila ya hewa, lakini ni kwa sekunde nne tu anaweza kuishi bila ya mtumaini. Kwanini? Hakuna nguvu kubwa kama nguvu ya matumaini. Hakuna ubishi kwamba maisha yamejaa changamoto nyingi za kutufanya tujikute tuna kata tamaa na kuvunjika moyo. Katika uzoefu wa maisha, kuna wakati fulani kila mtu atakabiliana na hali au jambo au mazingira ya kumfedhehesha, kumnyong’onyeza na kujikuta akijaribiwa kukataa tama na kusalimu amri. Tunapokutana na mambo hayo magumu tunaruhusiwa kupiga mayowe, tunaruhusiwa hata kulia machozi, lakini kuna jambo moja ambalo haturuhusi kabisa kulifanya, jambo hilo ni kukata tamaa. Ni marufuku kukata tamaa kwani kukata tama ni kupoteza matumaini yetu.
USIKATE TAMAA ,LIPO TUMAINI NI KITABU KILICHO BEBA JUMBE 18 ZA MATUMAINI ZENYE UVUVIO WA HALI YA JUU. UJUMBE ULIO KATIKA KITABU HIKI UNA NGUVU ZA KUMWINUA MTU YEYOTE ALIYEKATA TAMAA NA KUPOTEA MATUMAINI NA AKAONA BADO KUNA MATUMAINI KATIKA HALI YAKE.