KUFANYIKA KUWA KIONGOZI
Lengo la kitabu hiki ni kukusaidia uweze kugundua na kupalilia uwezo wa uongozi ulio ndani yako na ufanyike kiongozi yule ambaye Mungu amemkusudia. Ni matumaini yangu kitabu hiki kitakusaidia sana katika mchakato wa kukutayarisha, kukuandaa na kukukamilisha ili ufanyike kiongozi. rnKatika kitabu hiki utapata nafasi ya kujifunza masomo mbalimbali muhimu kama vile, maana ya uongozi, tofauti kati ya uongozi na usimamizi, msingi wa uongozi, kanuni za kiutendaji katika kiongozi, kanuni za kiutumishi katika Uongozi, na kanuni za kimaadili katika kiongozi. Ni maombi yangu kwamba, kwa kupitia kitabu hiki ule uwezo wa uongozi ulioko ndani yako utapaliliwa na kuchochewa na utapiga hatua moja zaidi katika mchakato wa kufanyika kuwa kiongozi.
KUFANYIKA KIONGOZI NI KITABU CHA MSINGI KWA KILA AMBAYE NI KIONGOZI. KUPITIA KITABU HIKI UNAWEZA KUJIFUNZA MAMBO YA MSINGI KATIKA UONGOZI NA KUWEZA KUENDELEZA UWEZO WA UONGOZI ULIO JIFICHA NDANI YAKO, NA HATA KUWA KIONGOZI YULE AMBAYE ULIKUSUDIWA KUWA.