Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Jinsi Ya Kuibua Ubunifu Ulio Ndani Yako - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

JINSI YA KUIBUA UBUNIFU ULIO NDANI YAKO

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
7,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 01, 2020
Product Views:
2,313
In category:
Sample

Mbinu Za 30 Kibunifu Zilizothibitishwa

Dhahabu inavutia kwa sababu ya mwonekano wake na thamani yake.  Leo hii ukigundua kwamba kwenye shamba lako kuna dhahabu basi  utajiri unakuwa umepiga hodi mlangoni kwako. Yaani ule usemi wa kulala masikini kuamka tajiri unakuwa umetimia kwako. Nani asiyependa dhahabu igunduliwe kwenye shamba lake? Ni nani huyo? Leo hii ninapoandika utangulizi wa kitabu hiki thamani ya dhahabu kwenye soko la dunia ni dola za kimarekani 38,000. Ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 86,723,600 (milioni themanini na sita laki saba ishirini na tatu na mia sita)!! Hii ndio dhahabu.

Sasa hayo yote yalikuwa ni tisa, ila kumi ni kwamba dhahabu kila mtu anaaweza kuitafuta na kuipata. Zipo kila sehemu. Na cha kushangaza zaidi ni kwamba dhahabu hizi hapa zipo karibu yetu sana. Dhahabu hizi hapa hatuzioni kwa sababu hatuzipi kipaumbele. Naam, dhahabu hizi zipo ndani yetu.

Kitabu hiki kimelenga katika kuhakikisha kwamba wewe unatumia dhahabu hii ambayo unayo ndani yako kwa viwango vya juu sana.

Je, dhahabu inayozungumziwa hapa ni ipi? Ni ubunifu ulio ndani yako. Na dhahabu hii inaweza kujitokeza kwa namna tofauti, inaweza kuwa ni kipaji cha kuzaliwa nacho, inaweza kuwa ni ujuzi ulio nao, inaweza pia kiwango chako cha elimu, hata biashsara unayoifanya.

Kama unaishi katika dunia hii basi nina hakika kwamba walau kuna kitu kimojawapo ambacho unacho  kati ya hivyo hapo nilivyotaja hapo juu na unaweza kukimudu kwa viwango vya juu kama utaamua. Ukweli ni kwamba una kitu na kama unaona kwamba hauna kipaji, ujuzi, kisomo cha kiwango fulani basi hapo kaa ujifikirie tena.  Hapo ndipo utagundua kwamba una kitu cha kuanzia na kitu hiki ni kimojawapo kati ya vitu hivyo hapo juu.

Sasa ukishajua kwamba upo wapi ndipo kitabu hiki hapa kinaingillia kati kwa kukutaka wewe uibue ubunifu wako zaidi ya hapo. Kitabu hiki hapa kinakutaka wewe hapo uweze kuupeleka ubunifu wako kwenye viwango vingine tofauti na sasa.

Usifanye kitu kwa sababu tu unafanya, bali ufanye kazi kwa kuongeza thamani zaidi kupitia ubunifu. Tumeona dhahabu unavutia watu walio wengi kwa sababu ya mwonekano wake, basi na wewe utawavutia watu wengi zaidi kwa kutumia ubunifu ulio ndani yako. 

More Products On Discount
7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

10,000 Tsh.
(0.8)

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold