KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI
DIBAJI Nimepata wasaa wa kusoma vitabu vingi sana katika maeneo ya maendeleo binafsi na ukuaji wa kifikra hata hivyo nikiri kwamba nilipokishika kitabu hiki nikasema wawooo! Nimejikuta nakisoma tena na tena, sio ili nipate cha kukisemea bali nimejikuta ninavutiwa na kuguswa mno na mpangilio, muundo na maarifa ya kina ambayo mwandishi ameyawasilisha. Mwandishi, ameingia katika orodha ya waandishi wachache na adhimu sana katika lugha ya Kiswahili, wanaoandika aina hii ya maarifa. Jambo kubwa la kujivunia katika kitabu hiki ni kwamba mwandishi amefanya utafiti wa kina na kuwasilisha maarifa kwa namna yake. Naweza kusema hiki ni kitabu kilichojipambanua mno kwa maana kwamba hakikufanyiwa tafsiri ya waliyoandika wengine bali kimeleta mawazo halisi na uvumbuzi wa mwandishi. Kongole kwa mwandishi! Ni hakika kwamba muda huwa haubadilishi chochote, bali unachokifanya ndani ya muda ndicho huamua mabadiliko utakayoyapata. Mwandishi katika kitabu hiki ameeleza kwa namna ya kipekee namna bora ya kutumia muda. Katika maisha kuna namna mbili za kufanikiwa. Ya kwanza ni kujifunza kwa kukosea na ya pili ni kujifunza kutoka kwa waliotangulia. Njia ya kwanza ni ndefu mno, maana utalazimika kugundua kila kitu wewe mwenyewe na itakuchukua muda mrefu. Njia ya pili ni fupi na itakuchukua muda mfupi sana kufanikiwa. Hata katika Biblia, mathalani, Mungu anasisitiza kwamba ni vema kuchukua muda na kuyatazama maisha ya waliotangulia ili kujipatia raha nafsini mwetu, yaani furaha na mafanikio ya maisha. Mwandishi katika kitabu hiki ameturahisishia mno, maana pamoja na uvumbuzi wake mwingi pia anatuletea hekima zilizounganishwa kutoka kwa rundo la waliofanikiwa katika maeneo mbalimbali. Mimi nimeandika vitabu takribani 11 hadi sasa katika maeneo ya uchumi na familia. Kwa uzoefu wangu katika uandishi wa vitabu ninakiri kwamba kitabu hiki kina upekee mkubwa sana tena wa namna yake. Ndio maana kitabu hiki nathubutu kukiita kuwa ni hekima nyingi ndani ya kapu moja. Utakapokisoma mwanzo hadi mwisho utathibitisha hilo. Mwandishi amefanya kazi nzuri mno kushughulika na vile mtu unavyoweza kuboresha hatma yako. Wale ambao huwa wanadhani mafanikio ni jambo la bahati nasibu, mwandishi anawanoa huo uvimbe wa fikra kwa msumeno wa maarifa ndani ya kitabu hiki. Ndio maana nimependa sana alipoeleza habari ya kujiingiza katika orodha. Ohoo, kumbe mafanikio sio bahati nasibu bali ni suala la kuamua, kutendea kazi uliyoyaamua na kupata matokeo. Suala la kupata mafanikio ni uamuzi wako binafsi na mwandishi anasema hujachelewa kabisa! Hiki ni kitabu ambacho ninapendekeza kisomwe kuanzia kwa vijana wadogo mpaka wazee. Kwa namna kitabu hiki kilivyo, kina hekima kwa rika zote. Kwa kuwa kina maarifa yenye chembechembe za kutengeneza na kuibua vizazi ni kitabu ambacho kinafaa kusomwa na watu wa elimu zote. Ingalikua amri yangu ningesema kitabu hiki kisomwe na kila mwanafunzi wa chuo kikuu, kisomwe na kila mfanyabiashara na mjasiriamali, kisomwe na kila mfanyakazi na kisomwe na kila mtu mahali popote alipo maadam anajua kusoma. Kuna mambo ndani ya kitabu hiki ambayo yakiingia na kupokelewa katika mioyo ya watu mahangaiko yatapungua sana kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja. Hongera kwa kushika nakala ya kitabu hiki, naamini muda utakaoutumia kukisoma pamoja na fedha uliyotumia kukinunua ni uwekezaji wa thamani sana na utakaokulipa vizuri sana maishani mwako na katika vizazi vyako vingi vijavyo Albert Nyaluke Sanga(SmartMind) Mwandishi & Mjasirimali Mwandishi wa vitabu kama: Gia Kubwa, Umeiweka wapi Talanta yako? na Barua Ya Siri kwa wanandoa miongoni mwa vingi alivyoandika hadi sasa.
WATU WANASEMAJE KUHUSU KITABU HIKI?
MIMI NAMFAHAMU GODIUS
Ninamfahamu Godius si tu kwa kupitia maandishi yake bali kwa kupitia
maisha yake. Jinsi anavyoishi ni darasa tosha la mtu yeyote mwenye nia ya kufanikiwa.
Nilipoanza kusoma kitabu hiki sikukoma kuacha kwani kimegusa maisha
yangu na baadhi ya mambo niliyoyapata humo nimeanza kuyafanyia kazi na nimeanza
kuona maajabu makubwa.
Unataka kuwa mbunifu? Soma kitabu hiki. Unataka kuwa kinara kwenye kipaji chako? soma kitabu hiki?
Unataka kuwa kiongozi kwenye maisha yako? Soma kitabu hiki.Unataka
maisha yenye furaha na ya kuacha alama? Majibu yote yanapatikana humu kwenye
Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni.
Imani yangu ni kwamba unaweza kuanzia hapo ulipo na kufika popote ili
mradi akili yako umeipa ruhusa. Kila mtu amezaliwa mshindi, hakuna aliyekuja
duniani kuwasindikiza wengine. Wewe ni wa tofauti, kuwa wewe, acha
kujilinganisha na wengine, kujilinganisha kunabagua.
Asante sana Godius Rweyongeza kwa kitabu hiki kinachotafakarishi,
kinachotia hamasa na kinachotupa dira ya kuishi maisha kwa utimilifu.
Edius Katamugora Mtunzi
Yusufu Nina Ndoto
MWANDISHI KATUMIA LUGHA NYEPESI KUONGEA
MAMBO MAKUBWA YA KIMAFANIKIO
Kila binadamu
ndani
kabisa
ya
moyo
wake ana tamanio kubwa la
kufanikiwa, yaani ikutoka ngazi ya
chini
kwenda
ngazi
ya
juu
katika
Nyanja mbalimbali za Maisha. Kwa lugha nyepesi “Kutoka
sifuri
mpaka kileleni.
Lakini
changamoto
kubwa
inayowakabili
watu
wengi
ni
njia
sahihi
za kupita au kanuni za kufuata ili kufikia
hatima
hiyo.
Mwandishi
Godius
Rweyongeza
amejaribu,
kwa kadri ya
uwezo
wake, kutumia lugha nyepesi
na
mifano
halisi
ya
kumsaidia
mtu
kuweza
kufuatana
kutimiza
azma
ya
mafanikio.
Amezungumza kiundani jinsi
ambavyo
binadamu
anaweza
kutumia
uwezo
wa
utashi
aliopewa na Mwenyenzi
Mungu
katika
kujiletea
maendeleo
binafsi
katika
Nyanja zote za Maisha.
Ni matumaini
yangu
kuwau
naposoma
kitabu hiki utaweka katika
matendo
yale yote utakayojifunza ili uweze
kupata
matokeo
bora yatakayokuwa chachu chanya
kwa
wengine
pia.
Nakutakia
usomaji
mwema
na
utekelezajiwa
yale yote utakayojifunza.
Anthony Luvanda
Mjasiriamali na Mhamasishaji.
KAMA
HUJUI NAMNA YA KUWEKA MALENGO, MWANDISHI AMEKUSAIDIA KUFANYA HIVYO KWENYE
KITABU HIKI.
“Usipowaambia watu kuhusu mafanikio yako bila shaka
hakuna atakayekuja kuyajua” Donald Trump
Acha Mimi nikuambie mafanikio yangu ili uyajue
kupitia kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Ukitaka kujua mafanikio
yako anza kusoma kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Kwani utagundua
uwezo mkubwa wa kufanikiwa ulioko ndani yako, kwanini unajichelewesha kupata
ushindi ambao uko ndani yako?
Kama hujui kabisa namna ya kuweka malengo hatua kwa
hatua ili yaweze kukusaidia kutoka sifuri hadi kileleni, basi mwandishi na
mtaalamu wa kilimo cha bustani (Horticulture) Godius amekusaidia kufanya kazi
hiyo kwenye kitabu chake cha kutoka sifuri hadi kileleni.
Ukiona mtu amefanikiwa kutoka sifuri hadi kileleni
jua kuna siri kubwa nyuma ya ushindi.
Ninapendekeza kila anayetaka kufanikiwa, na hajawahi
kusoma kitabu chochote kile basi kitabu hiki ni cha lazima kusoma kwa mtu
makini anayeanzia chini kabisa na kutaka kufikia kileleni. Ni kitabu
kinachokuonesha mchakato wa mafanikio
kutoka sifuri hadi kileleni.
Kila la heri rafiki yangu katika usomaji wa kitabu
hiki.
Mwl. Deogratius Kessy
Mwalimu, Mwandishi na Mjasiriamali.
HIKI NI
KITABU CHA KARNE YA 21
Kujitoa bila kujibakisha, kusimamia jambo bila ya
kurudi nyuma, pamoja na kugundua uwezo
wa ajabu aliouweka Mungu ndani yako, hivi vitakusaidia kufika hapo unapotaka
kufika.
Kitabu hiki
kimeanza kwa kwanza kwa kumsukuma mwandishi ujiuliza kwa nini wengine wamefika
walipokusudiwa na wengine hawafiki, majibu yake yakiwa ndani ya kitabu hiki,
yanagusa kuhamasisha na kufundisha, hiki ni kitabu cha karne ya 21,hivyo kila
mmoja anapaswa kukisoma.
Mwalimu Adebert
Chenche
Mwenyekiti wa
taasisi ya VIPAWA LINK ASSOCIATION
NI
KITABU CHENYE MAARIFA MENGI SANA.
Ni kitabu chenye maarifa mengi sana. Kwa uhakika
atakayekisoma na kuyafanyia kazi ataweza kupiga hatua kubwa katika kutimiza
malengo yake
NTANGEKI NSHALA