NAMNA YA KUIDHIBITI HOFU
Mwongozo wa kukusaidia kuanza kuishi maisha uliyoshindwa kuishi kwa sababu ya hofu
Watu wengi wanaishi maisha yao wakiamini kwamba hofu ni adui yao. Wanapoiogopa, hujaribu kuikimbia.
Lakini vipi kama tatizo sio hofu?
Vipi kama tatizo ni kwamba hatujaielewa vizuri?
Hofu haikuumbwa ili kukuharibia maisha.
Hofu ni mfumo wa tahadhari uliowekwa ndani yako kwa ajili ya kukulinda. Inapogundua uwezekano wa hatari, mwili na akili yako huanza kukuandaa kuchukua hatua.
Ndiyo maana unapokaribia kitu unachokiona kuwa hatari, unaweza kuhisi moyo kwenda mbio, mawazo kuongezeka, mwili kuwa na tahadhari na hata kutamani kukimbia.
Hapo ndipo tunapofanya kosa kubwa.
Tunachukua ishara ya tahadhari na kuitafasiri kama ushahidi kwamba hatuwezi.
Sasa unapaswa kujifunza kuhusu hofu kwa namna ya kipekee sana ambayo itakusaidia kuwa mtu wa tofauti utakaye anza kuthubutu kufanya mambo ya tofauti tofauti na mwanzo.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza